Majanga ya Asili

 

Ni Nini Kinachoendelea Duniani?

 

Yawezekana umegundua kwamba Sayari dunia inaonekana kukumbwa na matatizo makubwa siku hizi. Takriban kila juma tunasikia taarifa ya tetemeko jingine, moto, mafuriko au dhoruba vinavyoua maelfu, au makumi maelfu, au hata mamia elfu. Inahuzunisha sana. “Katika kila taifa misukosuko daima inaongezeka,” anasema Tina Brown, Mhariri mkuu katika gazeti la Newsweek. “Hivi dunia imechanganyikiwa?” anahoji.

Kwa kweli, hatuwezi kugundua jibu sahihi kwa kuangalia tu habari kwenye TV. Amini usiamini, sehemu pekee tunayoweza kuigeukia kwa ukweli wenye uhakika asilimia 100 kuhusu kwa nini majanga hayo ya kutisha yanaonekana kuongezeka siku hata siku kila pande za dunia ni kwenye kitabu cha kale ambacho unabii wake hutwambia kuhusu kizazi chetu.

Ni kitabu cha mwisho cha Biblia: kitabu cha Ufunuo. Angalia kwa umakini maelezo ya Ufunuo jinsi ambavyo kabla tu ya kurudi kwa Yesu Kristo mara ya pili—malaika wa mbinguni wanaelezewa kuwa wanazuia uangamivu wa ulimwengu: “Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote. Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.” (Ufunuo 7:1-3).

“Pepo nne za nchi” huwakilisha migogoro na vita vilivyoenea ulimwenguni, hasa majanga ya asili na “malaika wanne” wanaozuia pepo hizi huwakilisha nguvu za wema wa Mungu mwenye upendo ambaye hata sasa anazuia machafuko makubwa sana yasitokee. Lakini kwa kadiri tunavyoikaribia “siku ile kuu” ya Mungu Mwenyezi (Angalia Ufunuo 6:17), malaika hawa walinzi wa mbinguni mwisho huanza kuachia kushikilia nguvu zilizoshikiliwa za kifo na uangamivu-na ambazo mara nyingi zimevuviwa na Shetani. Hii ndiyo sababu majanga ya asili yanaongezeka kila siku.

Mwandishi mmoja wa Kikristo mwenye kugusa hisia alitoa maoni: “Hata sasa Roho wa Mungu anayezuia anaondolewa polepole ulimweguni. Dhoruba zenye nguvu, moto na mafuriko, majanga katika bahari na nchi kavu, hufuatana kwa haraka haraka. Sayansi hutafuta kuyaelezea haya yote. Ishara huzidi kuongezeka zikituzunguka, zikitwambia kukaribia kwa Mwana wa Mungu, zinaelezewa kuwa zinatokana na vyanzo vyovyote vile isipokuwa chanzo cha kweli. Wanadamu hawawezi kutambua malaika walinzi wanaozuia pepo nne kwamba zisiachiwe mpaka watumishi wa Mungu watiwe muhuri; lakini wakati Mungu atakapowaamuru malaika wake kuziachia pepo, kutakuwa na matukio ya ghasia ambayo hakuna kalamu inayoweza kuyaelezea.”

Maelezo hayo yanauelezea ukweli kwa ukamilifu kabisa. Wanasayansi waliopata mafunzo katika vyuo vikuu wanaweza kutoa maelezo mengine, lakini ukweli ni kwamba “majanga ya baharini na nchi kavu” yanayoongezeka huweka wazi kuwa “Roho wa Mungu anayezuia anaondolewa duniani hata sasa”. Lakini kwa nini? Binadamu wanafanya nini na kusababisha Mwumbaji wa mbingu na dunia kuondoa ulinzi wake kutoka kwa wale aliowaumba, anaowapenda na anaotafuta kuwaokoa? Jibu linashangaza, lakini ni rahisi. Katika kila sehemu duniani idadi kubwa ya wakazi wake – bila kujali matokeo yake ya milele, sasa wanaendelea kuvunja kwa wazi, na bila kujali, Amri za Mungu ambazo Biblia inasema “ziliandikwa kwa chanda cha Mungu” (Kutoka 31:18) katika mbao mbili za mawe. Katika Wafilipi 4:30, Paulo anaandika, “Msimhuzunishe Roho.” Hata hivyo leo hii bila dini, kila kitu ni chema, makundi makubwa ya watu wanaopenda anasa wanafanya hivyo saa 24 kwa siku saba za juma. Hii ndio sababu ya kweli kwa nini Mungu anaondoa mkono wake.

Kimsingi, hapa kuna Amri Kumi za Mungu katika lugha nyepesi:
1. Mtangulize Mungu kwanza
2. Usiabudu sanamu
3. Liheshimu jina la Mungu
4. Shika siku takatifu ya Sabato ya siku ya saba (Jumamosi)
5. Waheshimu wazazi wako
6. Usiue
7. Usizini
8. Usiibe
9. Usiseme uongo
10. Usitamani (soma kutoka 20:3-17)

Kwa mujibu wa kitabu cha Mungu, kuvunja Amri Kumi ni dhambi. “Dhambi ni uasi wa sheria” (1 Yohana 3:4), alithibitisha Yohana. Hata hivyo “Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee” (Yohana 3:16) ili kustahimili adhabu kamili ya sheria hii iliyovunjwa juu ya msalaba katili badala yetu. “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu” (1 Wakorintho 15:3) ni habari njema kutoka mbinguni. Kama tukiwa tayari kutubu, kuungama, na kuwa na imani katika Yesu kama Mwokozi wetu, “Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Wale ambao hufanya hivi katika nyakati hizi za mwisho—na hivyo kudhihirisha utii wao kwa kila amri katika Amri Kumi—watapokea “Muhuri wa Mungu aliye hai…juu ya vipaji vya nyuso zao” (Ufunuo 7:2,3). Pia watalindwa kikamilifu wakati “pepo nne” zitakapoachiliwa na “Ibilisi na Shetani” (angalia Ufunuo 2:9) atakapotwaa udhibiti kamili.

Kwa kadiri matetemeko makubwa, mawimbi makubwa, mioto isiyozuilika, mafuriko makubwa, dhoruba kali, vinavyoweza kuwa katili na kusababisha uharibifu mkubwa, hata hivyo Mungu analo kusudi kwa kuyaruhusu majanga haya kuiharibu dunia yake. Kwa ufupi, anajaribu kwa dhati kupata usikivu wetu. “Tubuni” ndio wito wake wa haraka katikati ya dhoruba. Lakini ni wachache tu ndio wanaosikiliza. Usomaji makini wa kitabu cha Ufunuo bado huelezea kuwa viongozi wa dini wanyofu lakini waliopotoka, hatimaye watatafsiri kimakosa matukio haya na kudai kuwa “Mungu anawaadhibu binadamu moja kwa moja kwa kukataa kwao kuishika siku ya Jumapili,” ingawa Amri Kumi kwa uwazi kabisa huelezea “siku ya saba” (Jumamosi) kama siku ya kweli ya mapumziko. Ikiwa itatokea umesikia tafsiri kama hizo za matukio ya sasa, usidanganyike kwa maelezo hayo. Soma Kutoka 20:8-11 na Ufunuo 14:12. Biblia huufunua ukweli.

Siku ya Jumapili usiku, mnamo tarehe 8 Oktoba, 1871, mwinjilisti mashuhuri aitwaye D.L. Moody alikuwa akihubiri mbele ya umati mkubwa huko Chicago kuhusu umuhimu wa wadhambi kujitoa kwa Yesu Kristo. ‘Wito wa kufanya maamuzi sasa!” ulikuwa ni mguso wa haraka wa Roho Mtakatifu kwa mhubiri. Lakini Moody alisita. Badala yake, aliuambia mkutano uliokuwa ukimsikiliza kuwa ataitisha wito wiki iliyokuwa inafuata. Kundi hilo halikurudi kamwe. Wakati wa wimbo wa mwisho sauti ya ving’ora vya magari ya zima moto vilisikika na kutangaza kuwa Moto Mkubwa wa Chicago ulikuwa umeanza. Uliwaka kwa siku mbili, na kuua mamia ya watu. Baadaye Moody alitamani sana kuwa heri angekuwa ametoa wito!

Msomaji mpendwa, majanga ya kutisha yanaweza kutokea wakati wowote. Kesho tunaweza kuwa tumekufa. Hata hivyo katikati ya huzuni na kupoteza maisha, Mungu anaumia pia, kama alivyoumia wakati Mwana wake wa pekee alipokufa msalabani. Kwa kututia moyo, neno lake linaahidi kuwa siku moja—wakati harufu mbaya ya dhambi itakapotoweka milele—hakutakuwepo na “mauti, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu. Kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita” (Ufunuo 21:4). Zaidi ya yote, hakikisha huikosi Mbinguni. Mchague Yesu Kristo leo!

 

<!-- Start of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) --><!-- [et_pb_line_break_holder] --><script type="text/javascript"><!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_project=11587914; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_invisible=0; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_security="4a09a56b"; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var scJsHost = (("https:" == document.location.protocol) ?<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"https://secure." : "http://www.");<!-- [et_pb_line_break_holder] -->document.write("<sc"+"ript type='text/javascript' src='" +<!-- [et_pb_line_break_holder] -->scJsHost+<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"statcounter.com/counter/counter.js'></"+"script>");<!-- [et_pb_line_break_holder] --></script><!-- [et_pb_line_break_holder] --><noscript><div class="statcounter"><a title="Web Analytics"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->href="http://statcounter.com/" target="_blank"><img<!-- [et_pb_line_break_holder] -->class="statcounter"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->src="//c.statcounter.com/11587914/0/4a09a56b/0/" alt="Web<!-- [et_pb_line_break_holder] -->Analytics"></a></div></noscript><!-- [et_pb_line_break_holder] --><!-- End of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) -->