Uhuru Unapotoweka
Uhuru, ni kitu cha thamani mno! Hata hivyo kinachohuzunisha, siku moja uhuru huu utaondolewa na watu, serikali, na mataifa. Hivi ndivyo itakavyotokea.
Isipokuwa kama hujui chochote kuhusu habari siku hizi, basi unagundua kuwa Sayari Dunia iko taabani–taabu kubwa. Majanga ya asili yenye kufisha, mifumo ya ajabu ya hali ya hewa, mashambulizi ya kigaidi, matatizo ya kiuchumi, kuporomoka kwa maadili, ufisadi wa kisiasa, kupanda kwa bei za vyakula, kupungua kwa upatikanaji wa maji na zaidi, yote huonesha kuwa tupo ukingoni mwa zahama kuu.
“Kutakuwa na wakati wa taabu,” hutabiri Biblia Takatifu, “mfano wake haukuwapo…” (Danieli 12:1). Wakati zahama ya mwisho ya dunia itakapolipuka, “ufumbuzi” wa uongo hatimaye utashurutishwa na serikali duniani kote wakati wa saa ya giza ya kukatisha tamaa. Kwa juujuu, ufumbuzi huu utaonekana kuwa mzuri kwa watu wengi. Lakini kilichofichwa ndani yake ni uongo kutoka kwa yule mwovu.
“Kutakuwa na wakati wa taabu,” hutabiri Biblia Takatifu, “mfano wake haukuwapo…” (Danieli 12:1). Wakati zahama ya mwisho ya dunia itakapolipuka, “ufumbuzi” wa uongo hatimaye utashurutishwa na serikali duniani kote wakati wa saa ya giza ya kukatisha tamaa. Kwa juujuu, ufumbuzi huu utaonekana kuwa mzuri kwa watu wengi. Lakini kilichofichwa ndani yake ni uongo kutoka kwa yule mwovu.
Kama ukitumia mtandao wa intaneti na ukatumia Google kutafuta maana ya “alama ya mnyama,” utapata maoni yasiyo na mwisho. Makisio yapo tele. Wengi huitafsiri kama alama ya kiteknolojia, lakini hii ni nadharia ya wanadamu tu. Biblia hufafanua zaidi kuwa “…aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama” (Ufunuo 19:20). Kwa hiyo wanaoipokea alama “hudanganywa,” au hufanyiwa ujanja, na matokeo yake ni upotevu wao wa milele. Sasa fikiria hilo. Endapo “alama” hiyo ya kufisha—vyovyote iwavyo—ingekuwa alama inayoonekana bayana, basi ingewezekanaje idadi kubwa ya wakazi wa dunia kupotoshwa, kama ambavyo Ufunuo hutabiri kwa uwazi?
Kwenye kijizuu hiki, ni kiasi hicho tu ndicho kinachoweza kusemwa. Hivyo, bila kuchelewa, ni muda mwafaka kwenda kwenye mada kuu. Tazama kwa ukaribu zaidi. Kwenye muktadha wa kuwaonya wanadamu kuhusu “mnyama” na “alama” yake ya kufisha (Ufunuo 14:9-11), kisha Neno la Mungu huonesha dhahiri wale ambao hawataipokea alama hiyo: wale ambao …humsujudia Yeye aliyeziumba mbingu na nchi… (Ufunuo 14:7).
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu (Ufunuo 14:12).
Je, umeelewa hilo? Wale wanaoishinda alama ya kufisha ya Shetani hufanya mambo matatu mahususi:
1) Humwabudu Muumba,
2) “Huzishika amri za Mungu,” na
3) Humwamini Yesu Kristo.
Ukiisoma Biblia kwa makini, utagundua kuwa ni amri moja tu miongoni mwa zile Amri Kumi ndizo “zilizoandikwa kwa chanda Chake” (tazama Kutoka 31:18) ambayo huzungumzia hasa kuhusu kumwabudu “Yeye aliyezifanya mbingu na nchi.” Ni Amri ya Nne, ambayo husema:
“Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa” (Kutoka 20:8 -11).
“Siku ya saba” ya juma ni Jumamosi, sio Jumapili. Chunguza kamusi, ensaiklopidia, au mwulize mtu yeyote ambaye ni Myahudi. Jambo la kushangaza kwa wengi ni kwamba Kanisa Katoliki—mfumo wa dini (sio Wakatoliki wenyewe) ambalo makanisa mengi ya Kiprotestanti hapo awali yalilitambulisha kuwa ndilo “mnyama,”—hudai waziwazi kuwa lilibadili Sabato ya Biblia toka Jumamosi kwenda “Jumapili,” inajulikana hivyo kwa sababu siku hiyo zamani ilitengwa kwa ajili ya ibada ya jua. Hebu jionee mwenyewe:
“Kwa kweli Kanisa Katoliki hudai kuwa badiliko [toka Jumamosi kwenda Jumapili] lilikuwa ni tendo lililofanywa na kanisa hili…..na kitendo hiki ni ALAMA ya mamlaka yake ya kikanisa juu ya mambo ya kidini.”—C.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons. Nov. 11, 1895 (Kiongozi wa Katoliki).
Mwulize kasisi yeyote. Tazama kwenye Katekisimu ya Katoliki. “Na tendo hili ni ALAMA ya mamlaka” ambayo hudhani kuwa yake, Roma hujivuna.
Fikiria hili: Wakati Majengo Mawili marefu ya Jiji la New York yalipoanguka baada ya kugongwa na ndege mnamo Septemba 11, 2011, tukio hilo la kutisha lilitokea Jumanne. Siku tano baadaye, mahudhurio ya kanisani Jumapili yaliongezeka sana, sio tu Marekani, bali katika dunia nzima. Kwa nini? Jibu linajulikana. Wakati zahama kubwa inapotokea, watu husali. Walikimbilia kanisani.
Hivyo, somo mojawapo kutokana na tukio hili la Septemba 11 ni kwamba zahama ya kutisha husababisha uamsho katika utunzaji wa Jumapili. Endapo tukio hilo la siku za nyuma lingekuwa kubwa kupita kiasi, kuongezeka kwa mahudhurio ya Jumapili hatimaye yangesababisha utekelezaji wa sheria za Jumapili duniani kote kwa kutumia serikali za kiraia.
“Haiwezekani!” baadhi ya watu wanaweza kudai. Hapana sivyo. Sheria za Jumapili tayari zimetekelezwa kwa viwango mbalimbali kule Ulaya, Uingereza, na Marekani kwa zaidi ya miaka 1,500 years.
Soma historia. Liulize Kanisa Katoliki.
Ndiyo, sheria za Jumapili zimewahi kutekelezwa siku za nyuma, na zitarejea tena kwenye zahama ya mwisho ya dunia nzima. Huku zikitekelezwa kwa jina la Mungu, sheria hizo kimsingi zitaikana sheria Yake na tabia Yake—kwa maana Mungu kamwe hamlazimishi yoyote amtii. Hutaka tu huduma ya upendo, sio utii wa kulazimishwa.
Jambo pekee linalozuia leo Sheria za namna hiyo za Jumapili ni zahama kali. Ni matukio gani yatakayoanzisha utimizwaji wa mwisho wa unabii wa Biblia? Ni Mungu pekee ndiye ajuaye. Huenda ikawa mfululizo wa majanga ya kiasili, shambulio lingine la kigaidi, kuanguka kwa uchumi, au mwunganiko wa matukio.
Wakati litakapotukia, kama ilivyokuwa kipindi cha Septemba, 11, 2001, mahudhurio ya Jumapili yataongezeka sana, ambayo hatimaye yatafuatiwa na upitishwaji wa sheria ya Jumapili. Hata jambo likiwa la kustaajabisha kama linavyosikika, usomaji makini na uliovuviwa wa Ufunuo sura ya 13 na 14, unatabiri jambo hili kwa usahihi, kwa hiyo hivi ndivyo litakavyotokea.
Wakati “alama” hiyo (uadhimishaji wa Jumapili) ya “mnyama” (Kanisa Katoliki) itakapotekelezwa kikamilifu na sheria (tazama Ufunuo 13:16) wakati wa zahama ya mwisho ya dunia, ndipo ile saa ya mwisho ya uamuzi itakuwa imewadia. Wale wanaouamini uongo huu (kinyume na Amri Kumi) watapigwa chapa ya dhambi “kwenye vipaji vya nyuso zao” (akili zao); wakati wale ambao hawatauamini, lakini wakiwa bado wanatii sheria ya Jumapili, watapigwa chapa kwenye mikono yao (matendo yao). Kinyume na makisio ya unabii wa uongo wa siku hizi, Mungu pekee ndiye atakayeona alama hii, sio wanadamu.
Hata hivyo unabii unatabiri kwamba watu wengi watamtambua yule mdanganyifu aliyejificha na kukataa kupokea alama hiyo. Badala yake, watamwabudu Muumba, “wakizishika amri Zake” na kumfuata “Yesu” (Ufunuo 14:12), Mwokozi wetu anayetupenda, aliyekufa kwenye msalaba ule katili kwa ajili ya dhambi zetu za kuivunja sheria ya Mungu (tazama 1 Yohana 2:2; 3:4), na akafufuka toka kwa wafu. “Mkinipenda,” Mwokozi wetu anasihi, “mtazishika amri Zangu” (Yohana 14:15). Wale ambao huzishika—kupitia neema Yake na uwezo Wake—watakuwa tayari kwa jili ya ujio Wake wenye utukufu (tazama Ufunuo 14:14-16) katika wakati wa “utimilifu wa dahari” (tazama Mathayo 28:20).
Rafiki mpendwa, wakati saa ya giza nene zaidi duniani inapofika, utafanya nini? Utampenda, utamwamini, na kumfuata Yesu, au utamtii mnyama? Katikati ya mkanganyiko ulioenea duniani kote, Muumba wetu anasihi:
“Nichague Mimi na siku Yangu!”