Imani yenye Maarifa?

 

Joel na Mark walikuwa marafiki wawili waliokuwa na imani tofauti kabisa. Joel alimwamini Mungu kama Mfalme mweza yote aliyeumba kila kitu ulimwenguni. Mark alikuwa mtu asiyeamini kabisa juu ya Mungu aliyedhihaki dini na kufikiri kuwa dunia yote—pamoja na yeye mwenyewe—vilitokana na ajali. “Unajuaje kuwa Mungu yupo na Biblia sio tu kitabu chenye visa vya uongo?” Mara kwa mara Mark alipinga. “Mungu yupo kwa sababu Biblia inasema hivyo na unaweza kuiamini Biblia kwa sababu ni Neno la Mungu,” Joel angemjibu hivyo. Kisha Mark angemcheka kuhusu hilo na kusema, “Hivyo ni sawa na kusema, ‘Mimi ni mtendakazi bora kwa sababu Frank amesema hivyo. Je, tunawezaje kumwamini Frank? Kwa sababu nasema tunaweza kumwamini.” Mantiki ya mzunguko iliyotolewa na Joel ina makosa na haitamshawishi mtu yeyote kuhusu uwepo wa Mungu au kwamba Biblia ni kweli. Hata hivyo bado wengi leo hawana sababu nzuri zaidi ya hapo kwa ajili ya imani yao katika Biblia. Je, kuna ushahidi wowote wa kweli unaothibitisha kuwa Biblia ni kweli? Je, maarifa na mantiki hutoweka pale watu wanapokuwa Wakristo?

NDOTO

Njia mojawapo ya kupima usahihi wa Biblia ni kuuangalia utabiri wake. Moja ya madai ya Mungu ni kwamba Yeye, kupitia Biblia, anaweza kuuelezea mambo ya wakati ujao (Isaya 46:9, 10). Kwa kuchunguza kumbukumbu za kihistoria za Babeli ya kale katika kitabu cha Danieli kutasaidia kujibu swali kuhusu usahihi wa Biblia. Hapa tunamwona mfalme anayeitwa Nebukadneza, mtawala ambaye habari zake zimeandikwa si tu katika Biblia, lakini pia katika kumbukumbu za kihistoria zingine za kihistoria. (1) Usiku mmoja aliota ndoto muhimu sana. Hata hivyo, alipoamka, hakuweza kuikumbuka ile ndoto—ila tu ilimsumbua. Aliwaita wenye hekima wake na kuwaamuru wamwelezee ndoto yake na tafsiri yake. Wenye hekima hao walistaajabishwa na ombi lake. Wakasema, “Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme…” (Danieli 2:10). Mfalme akaghadhibika sana akaamuru kwamba wenye hekima wote wa Babeli wauawe (Danieli 2:12). Hapa ndipo Mwebrania mmoja aitwaye Danieli anapoingia kwenye kisa hiki. Danieli alikuwa amechukuliwa kama mateka kwenda Babeli alipokuwa tu kijana mdogo. Danieli alikuwa akimwamini Mungu. Wakati Arioko, mkuu wa kikosi cha walinzi wa mfalme, alipomwambia Danieli kuhusu amri ya Mfalme, Danieli alikwenda kwa Mfalme na kumwomba ampatie muda ili aweze kumweleza ndoto yake na tafsiri yake. Mfalme akakubali. Danieli akaenda nyumbani na kwa moyo wa dhati akamwomba Mungu ili ampatie hekima. Mungu akajibu maombi yake na, ”Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku” (Danieli 2:19).

SANAMU KUBWA YA KIHISTORIA

Asubuhi iliyofuata Danieli akaenda kwa mfalme na kumfunulia ile ndoto. Mfalme alikuwa ameona sanamu kubwa. Ilikuwa na sehemu kuu tano tofauti. Kichwa kilikuwa cha dhahabu, kifua chake na mikono yake ni ya fedha, tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba, miguu yake ni ya chuma, na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. Kisha jiwe kubwa likaipiga ile sanamu na kuiseta vipandevipande vikawa kama makapi, nao upepo ukavipeperusha (Danieli 2:31-35). Ndipo Danieli akamwambia mfalme maana ya ile ndoto. Kichwa cha dhahabu kiliwakilisha ufalme wa Babeli (Danieli 2:38). Fedha iliwakilisha Uamedi na Uajemi; Shaba iliwakilisha Uyunani. Miguu ya chuma iliwakilisha Rumi. (2) Nyayo na vidole vya miguu vya chuma kilichochanganyika na udongo kiliwakilisha utawala ya Rumi uliogawanyika, nusu yake ukiwa na nguvu na nusu dhaifu. Kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyika na udongo, mataifa haya yasingeweza kuungana pamoja. Lile jiwe kubwa lililoipondaponda ile sanamu liliwakilisha ufalme wa Mungu. “Na… Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele” (Danieli 2:38-44).

KUTIMIA KWA NDOTO

Kila mmoja ya utabiri wa falme zilizowakilishwa na madini mbalimbali zilitimia kwa usahihi kabisa. Ufalme wa kwanza, Babeli, uliitawala dunia tangu mwaka 605 hadi 539 K.K. Taifa la Waamedi na Waajemi lilitawala tangu mwaka 539 hadi 331 K.K. Utawala uliofutia, Uyunani, ulitawala kuanzia mwaka 331 hadi 168 K.K. Dola ya Rumi iliyowakilishwa na chuma ilitawala tangu mwaka 168 K.K. hadi 476 B.K. Ufalme wa mwisho, uligawanyika katika falme ndogondogo nyingi, huwakilisha utawala wa Rumi iliyogawanyika, ambayo ni mataifa ya Ulaya kwa sasa, ambayo bado yamegawanyika mpaka leo. Biblia ilikuwa sahihi katika utambuzi wake wa falme zote tano na muda ambao zingeanza kutawala.

USHAHIDI MUHIMU ZAIDI

Watu wanaoshuku wamependekeza kuwa utabiri wa Danieli ni wa uongo, kitabu chake kimeandikwa baadaye zaidi katika historia. Hata kama hii ingekuwa sahihi, ukweli kuwa “Magombo ya Bahari ya Chumvi” yana machapisho nane kutoka katika kitabu cha Danieli, chapisho la zamani kabisa hukadiriwa kuwa la mwaka 125 K.K (3) (ambalo lenyewe pia ni nakala ya chapisho la awali zaidi), huonesha kuwa unabii huu uliandikwa miaka mia moja kabla Rumi haijagawanyika kuwa mataifa ya Ulaya ya sasa. Unabii huu ni mfano mmoja tu kati ya mia inayoweza kuoneshwa ili kuthibitisha kuwa Biblia imevuviwa na Mungu. Mfano mwingine mzuri unaonekana katika unabii wa Danieli sura ya tisa ambapo utimilifu sahihi wa ubatizo na kifo cha Kristo vilitabiriwa mamia ya miaka kabla ya matukio hayo. (4) Na hakika kweli, baada ya kuchunguza ushahidi kama tulionao kwenye unabii wa Biblia, tunaweza kufikia uamuzi kuwa tunaweza kumwamini Mungu na kuiamini Biblia! Sura ya pili ya Danieli hutuonesha jinsi ambavyo mojawapo ya unabii mbalimbali wa Biblia ulivyo wa kweli na sahihi, jambo linalotupatia msingi wa kuwa na imani yenye maarifa. Biblia ni neno la Mungu lililovuviwa na inaweza kuaminiwa kama mwongozo wetu katika kila jambo.

Hata hivyo, kuiamini tu habari hii kutaifanya tu iwe hivyo—habari. Kitendo cha kuamini peke yake hakina nguvu ya kuyaokoa maisha yetu. Lazima tubadilishwe kwa njia imani yetu katika ile kweli. Ni jambo lenye umuhimu wa milele siyo tu katika kuiamini Biblia, lakini kuiruhusu itubadilishe pia. Biblia inasema kwamba: “Mashetani nao waamini na kutetemeka!” Yakobo 2:19. Mungu atayachukua maisha yetu na kuyabadilisha kuwa kitu fulani chema ikiwa tutamruhusu. Je, utamruhusu?

1. Tafuta mtandaoni, katika Wikipedia, “Nebuchadnezzar II”

2. “The Next Super Power”—Mark Finley

3. “Maana ya “Dead Sea Scrolls” uk. 137, James C. VanderKam, Peter Flint.

4. “The Next Super Power”—Mark Finley

 

<!-- Start of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) --><!-- [et_pb_line_break_holder] --><script type="text/javascript"><!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_project=11587914; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_invisible=0; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_security="4a09a56b"; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var scJsHost = (("https:" == document.location.protocol) ?<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"https://secure." : "http://www.");<!-- [et_pb_line_break_holder] -->document.write("<sc"+"ript type='text/javascript' src='" +<!-- [et_pb_line_break_holder] -->scJsHost+<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"statcounter.com/counter/counter.js'></"+"script>");<!-- [et_pb_line_break_holder] --></script><!-- [et_pb_line_break_holder] --><noscript><div class="statcounter"><a title="Web Analytics"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->href="http://statcounter.com/" target="_blank"><img<!-- [et_pb_line_break_holder] -->class="statcounter"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->src="//c.statcounter.com/11587914/0/4a09a56b/0/" alt="Web<!-- [et_pb_line_break_holder] -->Analytics"></a></div></noscript><!-- [et_pb_line_break_holder] --><!-- End of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) -->