Je, Wafu Wanaweza Kuzungumza?

Je, wewe ni gari au kompyuta? Unasema, “Mimi si chochote kati ya hivyo. Mimi ni binadamu.”

Ni kweli, lakini hebu hata hivyo tuendelee kulichunguza swali. Magari na kompyuta zina kitu kimoja kinachofanana na sisi binadamu: sote tunahitaji maarifa ili tuweze kutenda kazi vyema. Hata hivyo, magari hayana akili zao yenyewe. Gari linahitaji dereva mwenye akili aingie ndani, awashe injini, na kisha aendeshe. Wakati dereva mwenye akili anapofika mwisho wa safari yake, huizima injini, na kisha gari “hufa.” Kisha dereva mwenye akili hutoka ndani ya gari hilo “lililokufa” na kuendelea na mambo yake.

Kompyuta iko tofauti. Maarifa yake yamo ndani yake. Hata hivyo, maarifa hayo huwa mfu, bila kufanya kazi mpaka kompyuta itakapounganishwa na chanzo cha nguvu ya umeme. Umeme unapoingia kwenye kompyuta, ndipo huwa “hai” na huweza kufanya shughuli zake za kiakili. Wakati nguvu ya umeme itakapokatishwa, maarifa ya kompyuta “hufa.” KOMPYUTA BADO INAMHITAJI MWANADAMU KUIUNGANISHA KWENYE UMEME.

Baadhi ya watu huamini kuwa, kama gari, maarifa yetu hutokana na roho iliyomo ndani ya miili yetu. Hii roho inandelea daima kuishi na haiwezi kufa, hivyo mwili unapokufa, roho huutoka mwili na kuendeleza kazi yake ya kiakili ikiwa mahali pengine. Watu wengine wanaamini kuwa akili yetu, kama ile ya kompyuta, imo ndani yetu. Hutokana na kazi ya seli za neva ndani ya ubongo wetu. Hata hivyo, kama kompyuta, ubongo unahitaji chanzo cha nguvu itokayo nje yake ili kuiwasha akili yake iweze kufanya kazi. Kisa cha uumbaji cha Biblia hutusaidia kuelewa jinsi sisi binadamu tulivyoumbwa—ama kama gari au kompyuta. Mwanzo 2:7 inasema, “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Zingatia vitu viwili. Cha kwanza, kama ilivyo kompyuta, mwili wa Adamu na wetu, pamoja na ubongo zetu, vimetengenezwa kwa vitu yakinifu, viwezavyo kushikika. Hata hivyo, ilikuwa ni baada tu ya Mungu kumpulizia Adamu pumzi ya uhai ndipo ubongo wake ulianza kufanya kazi na kiumbe hai mwenye maarifa. Huo ni mfano wa kompyuta, sio mfano wa gari.

Kifo ni kinyume cha mchakato huo. Kikizungumzia kifo, kitabu cha Mhubiri 12:7 inasema, “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.” Katika lugha ya awali ya Kiebrania iliyotumika katika kuandikiwa Biblia, neno “roho” limetafsiriwa kwa Kiswahili kama pumzi au upepo. Hivyo tunapokufa, Mungu huichukua pumzi ya uhai ambayo ilikuwa imewezesha bongo zetu, na akili zetu huacha kufanya kazi.

“Hebu subiri kidogo!” unasema. “Pumzi ya uhai inayomrudia Mungu ni roho.” Ni kweli kuwa Mungu huondoa kitu fulani kutoka kwetu tunapokufa, lakini vyovyote kitu hicho kiwavyo, sio maarifa, kwa sababu Mhubiri 9:5 inasema, “walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote.” Kwa hiyo, pumzi (au roho) hii ambayo humrudia Mungu sio sehemu yenye maarifa katika asili yetu.

Sisi wanadamu tuko kama kompyuta. Mungu anapotutia nguvu kwa kanuni yake iletayo uhai—pumzi ya uhai—tunakuwa wazima na akili zetu huanza “kufanya kazi.” Mungu anapoiondoa kanuni hii iletayo uhai, tunakufa, na akili zetu “huacha kufanya kazi—huzimika.”

Lakini, kuna umuhimu wowote?

Unaweza kuuliza, “Je, kuna faida gani kwangu sasa kuhusu jinsi ninavyopata akili yangu? Nitalifahamu hilo katika ile asubuhi njema kwenye ufufuo.” Kweli, sisi wanadamu hatupaswi kufahamu kama akili yetu ni kama ile ya gari au ya kompyuta. Hata hivyo kuna sababu ya muhimu sana inayotufanya tulazimike kujua, sasa hivi, jinsi tulivyoumbwa: sisi si viumbe pekee wenye maarifa tunaoishi kwenye sayari yetu. Biblia hutwambia kuwa miaka elfu nyingi iliyopita theluthi ya viumbe wenye maarifa wanaojulikana kama malaika waliasi na walifukuzwa kutoka mbinguni na kutupwa katika sayari yetu (Ufunuo 12:7-14). Tunawaita mapepo na mashetani. Mkuu wa malaika hawa walioasi aitwaye Shetani huwaongoza, na mojawapo ya malengo yao ya msingi ni kutudanganya (Yohana 8:44).

Yesu aliwaambia wanafunzi Wake kuwa mara tu kabla ya marejeo Yake ya pili makristo wa uongo wataibuka nao “watawadanganya wengi” (Mathayo 24:5). Miaka kadhaa baadaye mmojawapo wa wanafunzi wa Yesu, katika kipindi cha mwisho wa historia ya dunia, alisema “roho za mashetani, zifanyazo ishara, [zitatoka] na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi” (Ufunuo 16:14). Na mmojawapo wa wafuasi wa Yesu mwenye bidii zaidi, mtu aliyeitwa Paulo, alisema kitu hichohicho: “Yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa” (2 Wathesalonike 2:9, 10). Lakini miujiza ya Shetani idanganyayo ya siku za mwisho inahusianaje na hitaji letu la kujua chanzo cha maarifa yetu leo?

Umizimu

Bila shaka umeshasikia kuhusu umizimu. Kamusi ya Kiingereza ya Webster hueleza maana ya umizimu kama “imani kuwa wafu wanaendelea kuishi kwa njia ya roho zinazoweza kuwasiliana na walio hai…”* Watu wenye imani ya umizimu huamini kuwa, kama dereva wa gari fulani, sehemu ya akili ya asili yetu huendelea kuishi baada ya sisi kufa.

Imani hii imeenea sana katika ulimwengu wa leo. Vipindi vingi maarufu vinavyooneshwa kwenye TV na filamu huwahamasisha watu wauamini uongo huu. “Uthibitisho” mwingine maarufu juu ya maisha yenye akili baada ya kifo ni ule unaoitwa “uzoefu wa nje ya mwili” ambapo watu wanaokaribia kufa hudai kutoka kwenye miili yao na hupitia handaki fulani lenye giza hadi mahali pengine. Baada ya kuzungumza na marafiki waliokufa na wapendwa wao ambao wanaaminika kuwa wako mbinguni, hurudia miili yao iliyohusishwa na kutoa taarifa ya kile walichoona na kukisikia.

Halafu kuna uchawi, ambao pia unahusisha wazo la kuwa akili zetu huendelea kufanya kazi baada ya sisi kufa. Uchawi upo katika tamaduni zote katika namna mbalimbali, unahamasishwa na waganga wa kienyeji, filamu, TV, vitabu na njia zingine.

Inashangaza, wengi wa Wakristo wanakubaliana na wanaumizimu kuwa wanadamu wana roho isiyokufa ambayo huendelea kuishi baada ya mwili kufa. Hii hutoa fursa kubwa kwa mapepo kuwadanganya kwa kujifanya kuwa wapendwa wao waliokufa ambao wako mbinguni wakifurahi—wakati ukweli ni kuwa wapendwa wao wamekufa na wako kaburini wakiwa hawana utambuzi au akili yoyote ile.

Kadiri matukio ya mwisho wa historia ya dunia yanavyojidhihirisha wakati mfupi ujao, Shetani atatumia imani hii iliyoenea sana lakini isiyo ya Kibiblia kuwa wafu wanaweza kuwasiliana na walio hai kama sehemu ya ajenda yake ya kudanganya. Hii ndiyo maana ni muhimu sana uelewe ukweli kuhusu hali yetu ya kibinadamu katika kifo, leo. Itakuepusha usiweze kughilibiwa na mawakala wa kishetani, sasa hivi, na punde kabla ya kurudi kwa Yesu Kristo.

Mwisho, sababu moja nyingine kwa nini watu wengi wanapenda kuamini kuwa sisi ni sawa na gari ni kuwa lile wazo la kupoteza fahamu zetu tunapokufa huonekana kuwa la kutisha. Lakini maisha baada ya kifo hayategemeani na hali ya ufahamu wetu kuendelea kuwepo. Bali yanategemea kumpokea Yesu kama Mwokozi na kuamini ahadi Zake za kuturudishia tena uhai “katika ufufuo siku ya mwisho” (Yohana 11:24). Ninakutia moyo umwalike Yeye kwenye maisha yako leo na kuthibitisha ufufuo wako kwa ajili ya ufalme Wake wa milele. Je, utakubali?

 

 

<!-- Start of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) --><!-- [et_pb_line_break_holder] --><script type="text/javascript"><!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_project=11587914; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_invisible=0; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_security="4a09a56b"; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var scJsHost = (("https:" == document.location.protocol) ?<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"https://secure." : "http://www.");<!-- [et_pb_line_break_holder] -->document.write("<sc"+"ript type='text/javascript' src='" +<!-- [et_pb_line_break_holder] -->scJsHost+<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"statcounter.com/counter/counter.js'></"+"script>");<!-- [et_pb_line_break_holder] --></script><!-- [et_pb_line_break_holder] --><noscript><div class="statcounter"><a title="Web Analytics"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->href="http://statcounter.com/" target="_blank"><img<!-- [et_pb_line_break_holder] -->class="statcounter"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->src="//c.statcounter.com/11587914/0/4a09a56b/0/" alt="Web<!-- [et_pb_line_break_holder] -->Analytics"></a></div></noscript><!-- [et_pb_line_break_holder] --><!-- End of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) -->