Kesi ya Kiulimwengu

Mara chache mahakama za kibinadamu hugundua ukweli wote. Majaji na baraza la mahakama husikiliza ushahidi na kujaribu kutafuta ukweli kadiri wanavyoweza. Lakini fikiria hukumu ambayo kila kitu kipo wazi na sahihi. Hukumu ambayo huweka wazi kila tendo, kila kusudi, hata na kila wazo! Hiyo ndiyo aina ya hukumu ambayo Biblia inasema kuwa kila mmoja wetu ataikabili wakati maisha yatakapokoma. Hivi ndivyo Neno la Mungu linavyosema, “…sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu… Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu” (Warumi 14:10, 12).* Biblia inaongezea, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Waebrania 9:27). Kwa hiyo ni dhahiri kwamba, kila mmoja—watakatifu na wadhambi—watasimama mbele ya Mungu katika Siku ile kuu ya Hukumu. Kama wazo hilo linakuogopesha au kukunyima furaha, endelea kusoma.

Kile Biblia Isemacho Kuhusu Hukumu

Biblia iko wazi kwamba sisi sote tutaikabili siku kuu ya hukumu ya Mungu. Na itakuwa siku ya jinsi gani! Biblia huielezea: “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake… Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao” (Ufunuo 20:11, 12). Hukumu hii itachunguza kila sehemu ya moyo wa mtu. Yesu alisema hivi: “Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu” (Mathayo 12:36).

Biblia inasema kuwa Mungu “ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki” (Matendo 17:31). Na tunajua kuwa siku hiyo inakaribia sana. Muda si mrefu Mungu atafungua vitabu na kuhukumu kumbukumbu ya maisha ya kila mtu. Kwa kweli, Biblia iko wazi kuwa hukumu tayari imeshaanza mbinguni! Kitabu cha Ufunuo huelezea kwa uwazi kabisa malaika akisema kwa sauti kuu: “Mcheni [mwabuduni] Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja” (Ufunuo 14:7).

Yesu atakaporudi duniani mara ya pili, atakuja na ujira Wake mkononi (angalia Ufunuo 22:12). Waliokombolewa watapewa uzima wa milele, na waovu wataangamizwa. Kama ni hivyo, ni dhahiri kuwa uamuzi—hukumu—lazima iwe tayari imefanyika kabla Yesu hajaja kubainisha nani anayeokolewa na nani anayepotea. Hii awamu ya “upelelezi” ya hukumu kuu ya Mungu inaendelea sasa mbinguni katika maandalizi ya kurudi kwa Yesu duniani hivi karibuni.

Kwa nini hukumu ni muhimu

Hivi lakini Mungu si Baba wa mbinguni mwenye upendo? Kwa nini basi Biblia huonesha picha hii ya kuogopesha ya Siku ya Hukumu, na Mungu mwenyewe akiyachunguza maisha ya kila mtu katika kila kipengele? Kwa nini Mungu asimsamehe tu kila mtu na kuturuhusu sote tuingie mbinguni?

IIi kuweza kuelewa hitaji la hukumu, tunapaswa kuelewa kuwa Mungu ni wa haki na vilevile ni mwenye upendo. Ni vigumu, wakati mwingine, kwetu kuelewa kwamba haki na upendo ni pande mbili za shilingi moja. Kama mwanangu anampiga binti yangu, sitakuwa baba mwenye upendo mpaka nitakapofanya jambo fulani kuizuia hali hiyo. Na hiyo itajumuisha kumtendea haki mwanangu.

Ndivyo ilivyo kwa Mungu. Unaona, mtu fulani amekuwa akiwapiga watoto wa Mungu. Biblia humwita Shetani kuwa ni “simba angurumaye” akizungukazunguka akitafuta kutumeza (angalia 1 Petro 5:8). Alimwasi Mungu mbinguni, na anajitahidi kutushawishi kila mmoja wetu kujiunga naye katika vita dhidi ya Mungu.

Kwa upendo, Mungu anapaswa kushughulikia upinzani huu wa Shetani. Lakini kwa kufanya hivi humaanisha kuwa lazima aiangamize dhambi na wale wote wanaoendelea kuing’ang’ania. Na hiyo humaanisha kuuangalia ndani ya moyo wa kila mwanadamu. Kwa maneno mengine, Mungu anapaswa kufanya uamuzi—hukumu—kumhusu kila mtu. Anampenda kila mmoja wa watoto Wake; hataki yeyote apotee (angalia 2 Petro 3:9). Lakini kwa haki, na pia kwa upendo, lazima mwishowe Mungu awatenge wadhambi mbali na wale wote wanaompenda na kumtumikia Yeye. Hii ndiyo maana hukumu ni suala la lazima.

Hupaswi kuiogopa hukumu ya Mungu

Mjadala huu wote kuhusiana na hukumu unaonekana wa kutisha, sivyo? Inaogopesha kufikiria juu ya hukumu ambayo huchunguza kila wazo, kila kusudi, kila tendo tulilowahi kutenda. Tunajua kuwa maisha yetu hayakuwa makamilifu. Tuna nafasi gani ya kupitia hukumu ya namna hiyo bila ya kuhukumiwa?

Huu hapa kuna ukweli unaofariji: Yesu Mwenyewe ni Hakimu wako kwenye hukumu hiyo (angalia Yohana 5:22). Yule ambaye atakuwa Hakimu wako ndiye Yesu huyohuyo ambaye alikupenda kiasi cha kufa msalabani kwa ajili yako. Ndiye Yesu huyohuyo aliyemwambia yule mwanamke aliyekamatwa katika uzinzi, “Wala Mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena” (Yohana 8:11).

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya Hukumu

1. Tubu dhambi zako na ziungame mbele ya Mungu. “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako Kwake Bwana” (Matendo 3:19). Hatua ya kwanza ni kuzitambua dhambi zetu na kutubu—tuzisikitikie na kuziacha. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9).

2. Mwamini Yesu Kristo na umpokee kama Mwokozi wako akuokoe toka dhambini. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16; angalia pia Matendo 16:31 na 2 Wakorintho 5:19).

3. Mruhusu Yesu atende kazi ndani yako ili uishi kulingana na mapenzi Yake. “Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama Yeye [Yesu] alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu” (1 Yohana 4:17). “Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua Yeye [Yesu], ikiwa tunashika amri Zake” (1 Yohana 2:3). Uthibitisho kuwa umepokea kwa dhati neema ya Yesu iokoayo ni utayari wako kwa kumruhusu Yeye ayabadilishe maisha yako ili yaakisi tabia Yake. Yesu Mwenyewe alisema, “Mkinipenda, mtazishika amri Zangu” (Yohana 14:15).

4. Mwamini Yesu. Anasema, “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno Langu na kumwamini Yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani” (Yohana 5:24). Mtume Paulo analiweka kwa namna hii: “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 8:1).

Mungu anakupenda!

Ni kweli kwamba kama mdhambi, unastahili hukumu ya kifo katika siku ya hukumu. Lakini Yesu tayari amekufa badala yako. Ameichukua hukumu yako Yeye Mwenyewe na amelipa gharama ya adhabu ya dhambi zako. Kama ukikubali kile alichokufanyia na kwa imani ukamkubali Yeye kama Mwokozi wako—kama ukimruhusu aishi ndani yako na aiakisi tabia Yake maishani mwako—unaweza kuikabili hukumu bila woga.

<!-- Start of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) --><!-- [et_pb_line_break_holder] --><script type="text/javascript"><!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_project=11587914; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_invisible=0; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_security="4a09a56b"; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var scJsHost = (("https:" == document.location.protocol) ?<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"https://secure." : "http://www.");<!-- [et_pb_line_break_holder] -->document.write("<sc"+"ript type='text/javascript' src='" +<!-- [et_pb_line_break_holder] -->scJsHost+<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"statcounter.com/counter/counter.js'></"+"script>");<!-- [et_pb_line_break_holder] --></script><!-- [et_pb_line_break_holder] --><noscript><div class="statcounter"><a title="Web Analytics"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->href="http://statcounter.com/" target="_blank"><img<!-- [et_pb_line_break_holder] -->class="statcounter"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->src="//c.statcounter.com/11587914/0/4a09a56b/0/" alt="Web<!-- [et_pb_line_break_holder] -->Analytics"></a></div></noscript><!-- [et_pb_line_break_holder] --><!-- End of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) -->