Mwisho wa Ulimwengu?

Nyakati tunazoishi hazifanani na zozote zile ambazo tumewahi kuziona zamani. Viongozi wa nchi yetu, wafanyabiashara, watu wenye nyadhifa za madaraka na mamlaka, wote huangalia hali ya mataifa yetu—na ya ulimwengu—na wanajiuliza kitakachotokea baadaye. Kila mmoja anaangalia taarifa. Wanaangalia hali za machafuko katika jamii na mahusiano ya kimataifa, na wanaangalia majanga ya asili yakiharibu makazi na majiji, tangu maskini kabisa hadi kwa matajiri. Wanaumia kwa sababu ya taarifa za habari zinazoonesha kuporomoka ya maadili. Wanaonekana kuelewa kuwa mambo makubwa yanakaribia kutokea—mambo yatakayobadili mwenendo wa historia. Watu wanahitaji kujua: Je, tunaelekea mwisho?

Mara zote huonekana kana kwamba kuna nadharia mpya kuhusu wakati na jinsi ambavyo ulimwengu utafikia hatima yake. Muda mfupi tu kabla ya mwaka 2000, watu walikuwa wakisema kuwa ulimwengu ungelifikia ukomo mwaka 2000. Haikuwa hivyo. Halafu watu wakasema utafikia mwisho mwaka 2012. Kuna nadharia nyingi huko nje, lakini kamwe hakijawahi kuwepo kitabu zaidi ya Biblia kinachoaminika kutumika kwa utabiri wenye usahihi.

Unabii katika Biblia

Kuna mamia ya unabii katika Biblia ambao tayari umetimia. Wamisri wa zamani waligundua kabla wakati haujafika kuwa kungekuwa na miaka saba ya mavuno ikifuatiwa na miaka saba ya njaa kubwa katika Mwanzo 41. Taifa la Israeli liligundua katika Yeremia 25 kuwa kwa sababu ya kukosa kwao uaminifu, wangechukuliwa utumwani na taifa la Babeli. Jambo hilo lilipotokea, mfalme aliyewachukua mateka alipata ndoto, inayopatikana katika Danieli 2, iliyotoa unabii kuhusu mpangilio wa tawala za ulimwengu kuanzia wakati wake hadi mwisho wa dunia.

Miongoni mwa unabii wa Biblia uliotabiriwa kwa usahihi kwa kiwango cha kushangaza mno ni ule uliokuwa ukimlenga Yesu. Katika Danieli 9:25-27, tunaweza kusoma kuhusu wakati ambapo Yesu angelizaliwa na wakati ambapo angelikufa. Mafungu mengine kama Isaya 53:7 na Zaburi 22:7-8 pia hutabiri vipengele tofauti vya maisha ya Yesu.

Biblia na Unabii wa Siku za Mwisho

Ingawa tunaweza kuona aina nyingi tofauti za unabii katika Biblia, mojawapo ya unabii unaofahamika sana ni unabii wa siku za mwisho. Kuna vitabu viwili vyenye aina hii ya unabii kwa sehemu kubwa: kitabu cha Agano la Kale cha Danieli, na kitabu cha Agano Jipya cha Ufunuo. Kwa kweli, fungu 1 kati ya kila mafungu 25 katika Agano Jipya pekee hutaja ujio wa pili wa Yesu Kristo.

Kadiri Biblia inavyozungumzia mwisho wa ulimwengu na ujio wa pili wa Yesu, haituambii matukio haya yatakuwa lini. “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke Yake” (Mathayo 24:36). “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi [wakati wa usiku]…” (2 Petro 3:10). Lakini hutupatia maelekezo ya kuangalia wakati itakapokaribia. “Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita” (Mathayo 24:6). “Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi” (Luka 21:25-27).

Hapa Biblia hutupatia baadhi ya ishara za kutambua wakati tunapokaribia ule mwisho. Kutakuwa na majanga ya asili na vita, na watu watakuwa na hofu juu ya yatakayojiri baadaye. Lakini hayo siyo yote ambayo Biblia inasema kuhusu ule mwisho. Mathayo 24:24 hutuonya: “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.” Kwa hiyo, kulingana na Biblia, kutakuwa na zaidi ya uharibifu na machafuko ulimwenguni siku za mwisho, lakini pia hali itakuwa hivyo kwa upande wa kiroho.

Ni kusudi la Shetani kumdanganya kila mmoja anayeweza kudanganyika—na hatofautishi kati ya wale wanaokwenda kanisani na wale wasiokwenda. Hajali kama unajiita kafiri, Mkristo, Mbudha, au mmojawapo miongoni mwa wengine. Kwa kweli, Shetani hufurahia ikiwa unakwenda kanisani lakini huishi kulingana na kile unachojifunza. Ukiangalia kwa umakini visa vya Biblia, utaona kuwa watu wanaodai kumfuata Mungu lakini hawafanyi kile Bwana anachowaambia wana mwisho unaofanana na wale wanaokana kumjua Mungu. “Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua Yeye, ikiwa tunashika amri Zake” (1 Yohana 2:3)

Jinsi ya Kuwa Tayari kwa ajili ya Ule Mwisho

Kwa hiyo ni lazima tuulize swali: “Je, ni kwa namna gani naweza kuwa tayari kwa ajili ya wakati wa mwisho?” Biblia hutupatia maelekezo mengi jinsi ya kuwa tayari. Endapo tutayafuata kwa moyo wote, tunaweza kuwa na hakika kuwa tutakuwa tayari wakati Yesu atakapokuja tena.

Usidhani kuwa maelekezo haya hayakuhusu wewe. Yesu anatuonya mara nyingi sana katika aya za Mathayo 24 kwamba tusidanganyike. Kama lisingekuwa jambo linalowezekana hasa, huenda asingesisitiza. Mwisho wa ulimwengu utakuwa mgumu. Danieli 12:1 hutuambia, “na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo.” Haitakuwa rahisi, lakini Biblia pia hutupatia matumaini. “Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka” (Mathayo 24:13). “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja Nami katika kiti Changu cha enzi, kama Mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba Yangu katika kiti Chake cha enzi” (Ufunuo 3:21). Tunajuaje kuwa hatudanganywi? “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi” (Isaya 8:20).

Yatoe maisha yako yote kwa Yesu. Siyo tu sehemu hapa na pale. Mungu anaweza tu kusamehe dhambi ambazo unaziungama na kumpelekea. Hili ni jambo moja apendalo Shetani—watu wanaposema kuwa wao ni wa Mungu lakini wanaendelea kuishi jinsi watakavyo. Sisi pia hatupaswi kuliahirisha hili hadi wakati wa baadaye. “Angalieni, kesheni, ombeni, kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo” (Marko 13:33). Uwe tayari kwa ujio wa Yesu wakati wowote. Usijidanganye na kudhani kuwa hilo litatokea miaka 20 au hata miaka mitatu. Hakuna ajuaye—kwa hiyo kuwa tayari sasa.

Waambie marafiki zako. Tukio lingine hutokea kabla huo mwisho haujafika: wote watapaswa kuchagua watakayemtumikia. Mathayo 24:14 inasema, “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Mwishoni mwa wakati kutakuwa na makundi mawili tu ya watu: wale wanaomtumikia Mungu na wako tayari kumwona akija katika mawingu ya utukufu (Isaya 25:9), na wale wanaoangamizwa kwa mng’ao wa ujio Wake (Ufunuo 6:16-17).

Una chaguzi mbili tu za kufanya. Kubali mwaliko wa bure wa Yesu na uishi maisha yako kwa ajili Yake, au ishi maisha yako ukijifurahisha wewe mwenyewe—na ugundue mwishoni kuwa hayana thamani inayolingana na uzima wako wa milele. Mwisho wa ulimwengu si porojo tu: umekaribia, na utakuwa wakati wa taabu. Uchaguzi wako ni upi?

<!-- Start of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) --><!-- [et_pb_line_break_holder] --><script type="text/javascript"><!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_project=11587914; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_invisible=0; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var sc_security="4a09a56b"; <!-- [et_pb_line_break_holder] -->var scJsHost = (("https:" == document.location.protocol) ?<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"https://secure." : "http://www.");<!-- [et_pb_line_break_holder] -->document.write("<sc"+"ript type='text/javascript' src='" +<!-- [et_pb_line_break_holder] -->scJsHost+<!-- [et_pb_line_break_holder] -->"statcounter.com/counter/counter.js'></"+"script>");<!-- [et_pb_line_break_holder] --></script><!-- [et_pb_line_break_holder] --><noscript><div class="statcounter"><a title="Web Analytics"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->href="http://statcounter.com/" target="_blank"><img<!-- [et_pb_line_break_holder] -->class="statcounter"<!-- [et_pb_line_break_holder] -->src="//c.statcounter.com/11587914/0/4a09a56b/0/" alt="Web<!-- [et_pb_line_break_holder] -->Analytics"></a></div></noscript><!-- [et_pb_line_break_holder] --><!-- End of StatCounter Code for WordPress.org (I pay for<!-- [et_pb_line_break_holder] -->the hosting) -->